Maisha baada ya kuokoka...
Maisha baada ya wokovu - Je yanipasa kuishi maisha gani?
Ikiwa umepata wokovu, basi
yapo mambo ambayo inakupasha kuyafanya na kuyaishi. Jifunze juu ya mambo haya.
Mambo ya msingi
yakupasayo kuyafanya baada ya kuokoka
Ndugu yangu baada ya kuokoka
tu, kuna swali na amini liko ndani ya moyo wako, unajiuliza, sasa leo hii
nimeokoka nifanyenini sasa? Ni kweli ikiwa umeokoka kuna mambo
muhimu ambayo unatakiwa uanze kuyafanya, yapo mambo mengi sana,lakini ebu
nikupe haya mambo ya msingi ambayo unapaswa kuyafanya.
Jambo la
kwanza
===============================================
Jambo la kwanza
ambalo Mungu anataka kuliona kwako likitendeka baada ya kuokoka, ni
kukuona ukiukulia Wokovu. “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini
maziwa ya akili yasiyo ghoshiwa,ila kwa hayo mpate kuukulia wokovu;” (1PETRO
2:2)
Baada ya wewe kuhamishwa
kutoka katika ufalme wa giza na kuingizwa katika ufalme wa Nuru, yaani chini ya
utawala mpya ambao unataratibu tofauti na ule utawala wa kwanza ambao
inawezekana umeishi chini ya utawala huo kwa muda wa miaka mingi, Mungu anataka
akuone sasa ukianza kuyajua mambo mapya yaliyoko katika utawala
wake, anaposema kuukulia wokovu, maana yake kubwa ni
kuzidi kuyajua mapenzi yake Mungu, Uzidi kujua kwa upana
upendo wake kwako, uzidi kujua Uwezo wake ulivyo mkuu na nguvu zake zilivyo,
uzidi kujua ni nini umekusudiwa ukipate baada ya kuingia katika Ufalme wa Nuru,
ona maneno haya yasemavyo, “Kwa sababu hiyo mimi nami,tangu nilipopata
habari za imani yenu katika Bwana Yesu,na pendo lenu kwa watakatifu wote,siachi
kutoa shukrani kwa ajiri yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu, Mungu wa Bwana
wetu Yesu Kristo,Baba wa utukufu,awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika
kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, MJUE tumaini la mwito wake jinsi
ulivyo; na UTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHI WAKE KATIKA WATAKATIFU JINSI ULIVYO;
kwa kadili ya utendaji wa nguvu za uweza wake;…” (WAEFESO 1: 15-19)
Neno la Mungu linatufundisha
hapo kuwa Mungu anataka wewe na mimi baada ya kuokoka tu kwa njia ya
imani, tuanze kuyajua hayo mambo aliyoyataja Mtume Paulo na mengine
mengi, anataka ujue tumaini la wito wake jinsi ulivyo, Mungu amekuita baada ya
kukita amekukusudia nini? Anataka ujue baada ya kuokoka nini unachotakiwa
ukitalajie kutoka kwake, ujue baraka zako au haki zako ambazo Mungu amewa
ahidia kuwapa wale wote walio upokea huo wokovu, kwa mfano Baada ya wewe
kuokoka, Kuna kuna vitu ambavyo Mungu anakupa, anataka uvijue, angalia maneno
haya “Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono wangu wa
kuume,hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je! Hao wote si roho
watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale wataourithi wokovu!” (EBR 1: 13-14)
Neno la Mungu hapo
linatufundisha kuwa moja ya baraka amabazo walioupokea wokovu wanazipokea ni
hizi za kupewa wahudumu wa kuwahudumia, na wahudumu hao ni
malaika. Mtume Paulo alijua wazi kuwa kunamambo mengi ambayo Mungu
ameyakusudia kuwapa watu wote watakao urithi wokovu, akaamua kuwaombea hao
watu ili Mungu awasaidie kuyajua hayo yote, akawaombea hao ndugu
waliompokea Yesu kama Bwana na mwokozi wao wapewe Roho ya ufunuo wa
kumjua Mungu, pia akawaombea wapate ufahamu rohoni mwao wa kujua utajiri waliopewa
na Mungu baada ya kuokoka, pia macho yao ya ndani yaone kila kitu ambacho Mungu
anacho na amekiweka kwa ajiri ya watu wale walioamua kumpa Yesu maisha
yao.
Na amini umeelewa maana ya
kuukulia wokovu sasa, Sikia tena,unapozidi kujua ndipo unapozidi
kukua, au kwa lugha nzuri ndipo ufahamu wako wa kumjua Mungu unapokuwa mkubwa,
na hilo ndilo kusudi la Mungu kwako, anataka akukuze ufahamu wako katika kumjua
yeye na pia uyajue mapenzi yake kwa upana zaidi, angalia maneno yake haya ya semavyo
kuhusu jambo hili “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile
tuliposikia, hatuachi.kufanya maombi na dua kwa ajiri yenu,ili mjazwe maarifa
ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni” (WAKOLOSAI 1:9.) Mungu
anataka wewe ndugu upate kujazwa maarifa,hekima na ufahamu wa rohoni, mambo ya
rohoni ni mambo ya Kimungu, anataka ujazwe ufahamu wa mambo ya kimungu, Hiyo
ndiyo maana ya kuukulia wokovu.
Namna ya kufanya
Ili upate kukua au kuanza
kuyajua mambo hayo yote, unatakiwa uanze kuyanywa maziwa
yasiyoghoshiwa. Neno hilo lina maana maziwa yasiyochanganywa
na maji, mtoto mchanga azaliwapo, huwa hapewi chakula kigumu,
hunyonya maziwa ya mama yake, na kama akipewa maziwa ya ng’ombe au mbuzi, ni
lazima maziwa hayo yachanganywe na maji kidogo, hata wewe ili leo
hii uanze kuukulia wokovu inatakiwa uanze kunywa maziwa yasiyo changanywa na
maji, “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili
yasiyoghoshiwa, ila kwa hayo mpate kuukulia wokovu;” (1PETRO 2:2) Maziwa
hayo Neno la Mungu linayaita “maziwa ya akili”, au maziwa ya
ufahamu, unaweza ukawa na swali maziwa hayo nini? Maziwa hayo ni
Neno la Mungu, angalia maneno haya yasemavyo “ Ambaye tuna maneno mengi
ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa
kusikia. Kwa maana,iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita)
mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi
mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu kwa maana kila mtu atumiaye
maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni motto mchanga. lakini chakula
kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao kwa kutumiwa zimezoezwa kupambanua
mema na mabaya. ” (EBR 5:11-14)
Ukisoma maneno hayo
kwa kutulia utagundua wazi kuwa, Biblia inapozungumzia hapo kuhusu
maziwa inataja wazi kuwa maziwa ni Neno la Mungu, Kwa maana hiyo
kama unataka kuukulia wokovu unatakiwa uhakikishe unalitafuta neno la Mungu
iliutoke katika hali ya utoto na ukue. Hao ndugu walikuwa watoto kwa sababu
walikuwa wavivu wa kulisikia neno la Mungu, “ Ambaye tuna maneno mengi
ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa
kusikia.” (EBR 5:11) Kitu kilichopelekea hao ndugu
kukaa katika hali ya utoto kwa muda mrefu ni uvuvi waliokuwa nao wa kulisikia
neno la Mungu, Kama unataka kuukulia wokovu unatakiwa uhakikishe
unaondoa uvivu wa kulisikia neno la Mungu, neno la Mungu tunaweza kulisikia kwa
namna nyingi sana, Kwa kulisoma, Fahamu unaposoma unasikia, weka bidii kusoma
Biblia, kusoma vitabu mbalimbali ambavyo waalimu wa neno la Mungu wameviandika,
pitia tovuti (website) mbalimbali za watumishi wa Mungu, soma waliyoyafundisha
nenda kayahakikishe kwenye Biblia yako kama ni sahihi. Pia unaweza
kusikia mafundisho kwa kupitia semina,mikutano, ibadani kwenu, hata kwa kununua
kanda za mafundisho ya neno la Mungu, cd.au vcd ama dvd nk. Ukiweka bidii
katika kusikia fahamu hata imani yako kwa Mungu itakuwa kubwa sana, pia ufahamu
wako wa Mambo ya Mungu utaongezeka siku hata siku. Ndani ya neno la Mungu huko
ndiko kuna maarifa na ufahamu wa kumjua Mungu na kumcha. Sikiliza haya maneno
ya Mungu yasemavyo“ Mwanangu. Kama ukiyakubari maneno yangu na kuyaweka
akiba maagizo yangu; hata ukatega sikio lako kusikia hekima, ukaelekeza moyo
wako upate kufahamu; naam ukiita busara na kupaza sauti yako upate ufahamu;
ukiutafuta kama fedha, na kuutafuta kama hazina iliyositirika; ndipo
utakapofahamu kumcha Bwana, na kupata kumjua Mungu.” (MITHALI 2: 1-5)
Ili
leo hii upate ufahamu, upate kujua kumcha Mungu, lazima uweke bidii ya
kulitafuta neno la Mungu kama vile unavyotafuta fedha, kama unabidii kubwa ya
kutafuta fedha bidii hiyo hiyo unafundishwa uiweke katika kulitafuta neno la
Mungu, ndani ya neno la Mungu huko ndiko kuna maarifa yote, ili leo hii upate
kuishinda dhambi yapo maarifa ndani ya neno la Mungu, ili leo hii upate
kubarikiwa, maarifa ya kubarikiwa yapo ndani ya neno la Mungu, neno la Mungu
ndio dila ya maisha yote atakayo Mungu uyaishi ukiwa hapa duniani, Mungu
ameweka siri zake humo ndani ya neno lake. Ili uendelee kuokolewa kila siku
maarifa yake yamo ndani ya hilo neno la Mungu, inawezekana ukawa na swali hili
ikiwa nimekosea baada ya kuokoka ninatakiwa nifanyenini?, Sikia maarifa hayo
yamo ndani ya neno la Mungu sikia neno lisemavyo “ Watoto wangu wadogo,
nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye
mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi
zetu; wala si kwa dhambi zetu tu,bali na kwa dhambi za ulimwengu wote” (1YOHANA
2:1-2) Weka bidii ya kulisoma neno la Mungu,na kulisikia hapo
ndipo utakapo ukulia wokovu. Naamini umeelewa jambo la Kwanza.
Jambo
la pili
===============================================
NI
KUOMBA AU (KUZUNGUMZA NA MUNGU)
Jambo la pili muhimu ambalo
unatakiwa ulifanye ni kuomba. Nini maana ya kuomba? Kuomba ni kuzungumza au
kushirikiana na Mungu, Mungu anataka kushirikiana na wewe, Kumbuka ulipo okoka
alilejeza ushirikiano kati yake na wewe, kwa hiyo anataka kuudumisha ushirika
huo, na ushirika huo utaudumisha kwa kupitia maombi, Neno la Mungu linasema
hivi “Haya njooni tusemezane,asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu
sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera,zitakuwa
kama sufu” (ISAYA 1: 18). Mungu anataka kusema nawe, na amekupa kibali
cha wewe kwenda kuzungumza naye, ameamua kukusamehe, na baada ya
kukusamehe,amekupa nafasi ya kusema naye, tunasema na Mungu kwa njia ya
maombi.
Baada ya kumpokea Yesu
fahamu yuko ndani yako, hayupo mbali na wewe yuko karibu, anachotaka ni wewe
kumshirikisha kila jambo, ukiwa unauhitaji fulani anataka umwambie
akusaidie, angalia maneno haya ya Mungu yanavyotufundisha, “
Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini, upole wenu na ujulikane
na watu wote. Bwana yu karibu. msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila
neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na
zijulikane na Mungu” (WAFILIPI 4:4-7)
Mungu anataka
umshirikishe kila unacho hitaji, hapendi kukuona wewe ukijisumbua peke yako,
anataka ushirikane naye umweleze kila kitu, usimfiche ikiwa umekwama katika
kona fulani mweleze nk. Hata ukikosea omba maombi ya kuomba msamaha,
atakusamehe, ikiwa unaumwa omba uponyaji atakusaidia, ikiwa unashida yoyote ile
mwambie, atakusikia kwa kuwa hayupo mbali nawe, kumbuka yupo karibu sana na wewe
kuliko vile unavyo fikiri. Unaweza kuwaza moyoni mwako kuwa mimi sijui kuomba,
sikiliza hakuna anaejua kuomba. Neno la Mungu lina sema hivi, “Kadharika
Roho naye hutusaidia udhaifu wetu,kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo;
lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, naye
aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama
apendavyo Mungu.” (WARUMI 8: 26-27)
Mimi na wewe hatujui
kuomba. Neno la Mungu linasema wazi hapo, wewe anza kuomba tu,
usiogope kuwa utakosea, ondoa wazo kuwa Mungu anawasikia watu Fulani tu, Mungu
anamsikia kila mtu aliye na imani kwake, na ambaye hamfichi dhambi zake,
kumbuka anasema njooni tusemezane, amekuahidi kukusafisha dhambi
zako zote, hata kama ni nyekundu sanaa, anachotaka ni hiki, usimfiche maovu
yako, ziungame dhambi zako zote mbele zake, atakusamehe,ndipo umuombe, na
ukimwomba atakupa hicho umwombacho, kama unataka kuukulia wokovu,
weka bidii katika eneo hili la kuomba. Kinachotakiwa ukifanye kwenye
maombi yako omba kwa Jina la Yesu Kristo. Usisahau kulitumia jina hili katika
maombi yako, ili maombi yako yashughulikiwe mbinguni, lazima uyagonge muhuli wa
jina la Yesu Kristo. Bwana Yesu anatufundisha kuhusu habari za maombi
anasisitiza sana kuhusu jambo hili la kuomba, na anapo tufundisha kuomba
anatutaka tunalitumia jina la Yesu katika maombi yetu. “ Tena
siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin,
nawaambia,mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu. Hata
sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni nayi mtapata; furaha yenu iwe
timilifu” (YOHANA 16:23-24)
Jifunze kulitumia jina la
Yesu katika maombi yako, pia jifunze kuwasamehe watu wote waliokukosea kabla
hujaingia kwenye maombi. Neno la Mungu lina sema hivi “ Nanyi kila msimamapo
na kusali,sameheni mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni
awasamehe ninyi makosa yenu. (Lakini kama ninyi hamsamehe,wala Baba
yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu)”
(MARKO
11: 25-26). Jifunze kuwasamehe watu wote waliokukosea kabla
haujaingia kuomba, kwa kufanya hivyo utajikuta unafanikiwa sana katika eneo
hili la kushirikiana na Mungu kwa njia ya maombi. Hili ni jambo Muhimu
katika habari za kuukulia wokovu ulioupokea.
Jambo
la tatu
===============================================
Jambo la tatu ni hili,
waambie watu wegine kuwa umeokoka. Sikiliza ikiwa leo hii unataka Mungu azidi
kukukuza katika wokovu unatakiwa ujifunze kumkiri Yesu kwa kupitia kinywa chako
kama Bwana na mwokozi wako, sikiliza maneno haya yanavyotufundisha. “Kwa sababu
ukimiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa bni Bwana, na kuamini moyoni kuwa Mungu
alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu uamini hata kupata
haki,na kwakinywa hukiri hata kupata wokovu” (WARUMI 10:9-10). Maneno
hayo ya Bwana yanatupa maarifa makubwa sana, unatakiwa uamini moyoni mwako na
pia uanatakiwa ukiseme kile ulichokiamini anasema wazi kuwa ili uupate wokovu
inakusapasa ujifunze kuamini moyoni kuwa Yesu ndiye Bwan mwokozi wako, na pia
ukiri au useme kwa kinywa chako kuwa Yesu ndiye Bwana na mwokozi
wako, ikiwa leo hii umempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako
usiogope kuwambia watu wengine kuwa UMEOKOKA!. Ukifanya hivyo ndipo unapoumbiwa
wokovu kila siku, kwanini useme? Sikiliza Mungu anaumba matunda ya kinywa
chako. “Mimi nayaumba matunda ya midomo” (ISAYA 57:19A).
Mungu ana tabia ya kuyaumba
yale uyasemayo, sasa ikiwa leo hii utaanza kukiri au kusema Yesu ameniokoa,
ndipo Mungu atapo umba wokovu kwako! Umeona hilo jambo la tatu lilivyo muhimu?
Kama leo hii hutaki kwenda mautini, lazima ujifunze kuumba pamoja na
Mungu wokovu wa kukutoa mautini. Unaweza kujiuliza nitaumbaje pamoja na Mungu?
Sikiliza Mungu anayaumba yale uyasemayo, ukisema umeokoka kutoka
mautini na Yesu ndiye mwokozi wako, fahamu ndipo utakuwa unaumba wokovu huo pamoja
na Mungu, kwa kuwa Mungu anaumba yale tuya semayo, ebu angali maneno haya
yasemavyo. “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao wa upendao
watakula matunda yake.” (MITHALI 18 : 21). Kuna nguvu kubwa sana ya
uumbaji kupitia maneno uyasemayo, neno la Mungu hapo linasema mauti na uzima
huwa katika uwezo wa ulimi. Yaani kile unachokisema ndicho kitakacho kupa Uzima
au mauti, iwapo utaanza kusema kuwa umeokoka, basi fahamu ndipo utakapokuwa
unaumba uzima katika maisha yako . Basi ndugu yangu mpendwa
ikiwa umeokoka usisite kusema kwa watu kuwa umeokoka! Hapo utakuwa
unaukulia wokovu.
Na amini kwa sehemu
umefahamu ni mambo gani muhimu unayotakiwa uyafanye baada ya kuokoka, ya fanyie
kazi na ndipo utakapo ukulia wokovu, Mungu Yesu Kristo akubariki sana.
by willy m.samlega
No comments:
Post a Comment