Monday, December 9, 2013

LIFE OF APOSTELS AND THEIR DEATH/ MAISHA YA MITUME NA VIFO VYAO

MAISHA NA VIFO VYA MITUME WA BWANA YESU KIRISTO.


YESU ALISEMA MTU AKITAKA KUMFUATA SHARITI AJIKANE MWENYEWE NA KUUBEBA MSALABA WAKE NDIPO AMFUATE:MATHAYO 16:24 SOMA WAFILIPI 1:29 1PETRO 4;14

MTUME PETRO.

Mtume Petro a lipata mateso makalili  aliya pata kwa kusulubiwa kichwa chini miguu juu, hii ni adhabu aliyo I chagua yeye baada ya kushitakiwa kwa ajili ya kumhubili bwana yesu. Hakutaka  kusulibiwa kama yesu kiristo.

MTUME YOHANA (YOHANA NTAKATIFU)

Mtume huyu alipendwa sana  na bwana yesu kwa mjibu wa bilbilia na vitabu mbalimbali kama histoaria ya kanisa, bibilia ya mafunzo ya uzima tele, pia comentally  ya bibilia, bible dictionary,
Ni mtume pake yake aliye kufa kifo cha kawaida, ila alipitia majilbio kadha wa kadha ya kumuua,
>mtume huyu aliwekwa kwenye pipa la mafuta yanayo chemuka lakini  alitoka hai,
>mtume huyu alikatwa kichwa bila mafanikio ya watesaji  bila kukatika shingo yake
>Alifungwa nyasi mwili mzima  na kuchomwa moto, nyasi ziliungua lakini yeye na nguzo zake hakuungua
>Alipigwa mawe mpaka  walipo lizika na kuzani amekufa lakini aliinuka na kuendelea na shughuli zake kama kawaida
>kaisari Domatian aliamua kumtupa katika kisiwa cha  patimo, ili afe huko kisiwa kilikuwa kimejaa  barafu na baridi  lakini hata hivyo  mtume yohana hakufa badala yake akapata  ufunuo wa kitabu cha ufunuo wa yohona. Jambo lamaana ni kwamba mtume yohana akiwa patmo alipwe ufunuo,wakati maadui wa injili walio dhani baridi na njaa vitamuua mtume yohona matokeo yake ni kupata  ufunuo wa mbiguni. Inasemekana mtume yohana baada ya kuhubili  injili huko efeso alikufa kifo cha kawaida tu huko efeso.

MTUME YAKOBO

Mtume yakobo nimutume wa wanza kuuwawa na ndiye mtume pekee ambaye habari za kifo chake zimeandikwa katika kitambu cha matendo ya mitume.
>mtume huyu alishitakiwa kwa mashitaka ya uongo kisha  wakampeleka mahali pa kukatwa kichwa  kwa upanga. Jambo la kutia moyo katika historia hiyo ni pale  Yule mtu laliy jitolea au aliye pedekezwa na heredo kutoa mashitaka ya uongo. Aliamua kumsindikiza mtume yakobo akiwa anakwenda  kuuwawa baada ya kuona muonekano wa mtume yakobo ni tofauti  na vile alivyo tarajia.kwani alitalajia kuwa angekuwa mnyonge, mwenye hofu na mashaka lakini matokeo yake  mtume yakobo akawa mwenye furaha kuu akiimba nyimbo za kumsifu mungu.yule mtoa mashitaka ya uongo alipo ona hayo alishikwa na hofu kuu na kuamini kuwa kweli mungu yu pamoja na mtume yakobo.wakati wa kuuwawa kwake,yakobo aliona uso wake uking’aa kwa furaha kuu ndipo naye akaamuua kumpokea bwana na kutangaza kuwa naye ameokoka . wote wawill walikatwa vichwa siku moja kwa upanga ule ule.

MTUME MATHAYO

Mtume huyu mathayo ni Yule ambaye alikuwa mtoza ushurumaliko 2:14 mthatyo 9:9 mtume alihubiri maeneo mbalimbali,kama jelusalem, Ethiopia, iran,
> mtume huyu aliuwawa kwa kukatwa kichwa chake.

MTUME PHILIPO

Mtume philpo alihubili maeneo mbalimbali, aliuwawa kwa kusulubiwa msalabani

MTUME ANDREA

Kuhusu huyu mtumishi soma yohana 6:9 yohana 12:22
Mtume huyu alihubili injili katika inchi ya ugiliki , alikufa kwa kusulubiwa kwa msalaba wa x yanimbao mbili zilisimikwa chini ya andrea akaangikwa ili afe polepole. Walimfunga kwa kamba ilichukua muda wa siku tatu akafa.

MTUME YUDA WA YAKOBO

Mtume huyu likuwa akihubili injili nakufanya miujizaa alichukiwa kwa chuki kuu na wa Armenia wakamkamata na kumsulubisha. Akiwa msalabani wakamchoma mkuki akafa.

MTUME SIMON MAKANYO

Mtume huyu alikuwa akifany akazi ya kuhubili injili aliwa huko uajemi aliuwawa.

MTUME BATHALOMEYO

Mtume huyu ni moja ya wanafunzi wa mwanzo wa bwana yesu,alihubili injili kama vile india,pathia, Arabia na Armenia, alipo kuwa huko Armenia ndipo alipopata mateso mengi sana kwaajili ya imani ya kiristo na jina la yesu, mtume huyu alikuwa na mke mumoja na watoto wawili wa kike.mmoja alikuwa ni muombaji na mwingine alikuwa mwimbaji.mtume bathelomeyo alivuliwa nguo zote huko armania na kukatwa mshipa wa damu kwenye mkono wake. Kasha damu yake ilikingwa kwenye glasi mbili na kupewa mkewenye  mkewe ambaye alikunywa na baada ya kumaliza kunywa damu ya mume wake akasema maneno yaha “mume wangu jipe moyo mimi natangulia kwa baba”kasha baada ya kusema hayo akaangunguka chini akafa.
>Vile wale mabinti wawili walipewa glasi moj moja ya damu ya babayao nao wakasema “baba  jipe moyo sisi tunatangulia kwa baba”nao pia wakafa mumoja mumoja.
>baada ya zoezi hilo kumalizika wakaamuua mtume bathelomeyo toka pale alipolala na kuanza kumchuna ngozi yake, baada ya juchuna ngozi yake yote  inasadikika alikuwa bado hai hivyo wakaamua kumtundika msalabani, baada ya kuona kwamba hajafa waliamua kuchukua na kumtumbukiza kwenye pipala mafuta ya moto.

MTUME YAKOBO (aitwaye mdogo)


Mtume  huyu yakobo anaitwa mdogo ilikutofatisha kati ya yakobo ndugu yake yohana,kifo chake imeonekana katika kitabu cha matendo sura ya 12, alikuwa akihubiri yelusalem.
>aliuuwawa kwa kupigwa mawe huko jelusalem na wayahudi.

MTUME YUDA ISAKRIOTE

Mtume huyu alijinyonga baada ya kuisaliti damu isiyo na hatia,nafasi yake ilichukuliwa na mtume mathia.

MTUME MATHIA

Mtume huyu aliuwawa kwa kupigwa mawe akiwa huko kolosai katika huduma ya injili.

MTUME PAULO

Mtume huyu ni maarufu sana katika miongoni mwa mitume, alipata mateso mengi sana mara nyingi kama kupigwa viboko 39, kufungwa gerezani, kupigwa mawe,
>mtume huyu aliuwawa kwa kukatwa kichwa chake huko rumi.

MWINJILISTI MARKO

Mtumishi huyu aliuwawa kwa mateso kwani alikuwa akifanya huduma ya injili huko misiri, wamisirli walimuonea wivu na kumkamata, kasha wakamfunga kamba miguu yote miwili kisha  wakaanza  kumburuza barabarani. Kichwa kilikuwa chini na mgongo ukiburuzika chini na ukiendelea kuchubuka na kuchuruzika damu.baada ya mateso hayo makali wakamfikisha gerezani akiwa nyama zake zimekwisha katika mwili wake, kisha wakamuweka gerezani ambako walimwangia mafuta na kisha kumchoma moto.huo ndio ukawa mwisho wa maisha ya mwinjilisti marko.

MWINJILISTI LUKA (Dr Luka)

Dr luka yeye alikuwa tabibu, mtumishi huyu wa mungu inasemakana alifanya kazi ya kuchunga makanisa na kuhubiri sehemu mbalimbali, mtumishi huyu haijulikana kwamba alikufa kwa kifo gani na wapi inasadikika aliasilika na mateso ya kanisa chini ya mfalme nero wa dola ya rumi.

MTUME YAKOBO (NDUGU YAKE BWANA YESU)

Mtume yakobo ni ndugu wa kunyonya wa bwana yesu mathayo 13:55.  Mtume huyu alikuwa anafanya huduma yake katika mji wa yelusalemu aliuwawa kwa kupigwa kwa mawe baada ya kupandishwa juu ya mnara wa hekalu la yerusalemu na kuambiwa ajiangushe chini.

MTUME STEPHANO

Alipigwa kwa mawe mpaka kufa, na sauli ambaye ni Paulo alikuwa akishuhudia kifo cha stephano huyu ni moja wa mashahidi wa imani.
Mwangalie ayubu katika mateso yote hakumwacha mungu, Daniel, misheck shadraka na abinego hawa kumwacha mungu, waliinua macho juu ambako msada wa mungu unatoka.
Unaweza kusoma zaidi katika bibiliaya mafunzo ya uzima tele, hollman illustrated bible dictationary,simith bible dictionary

Nb:  naamini kwa kusoma habari ya watumishi wa mungu utapata hatua ya kwenda mbele kiimani bira kumwacha yesu. Yesu mwenyewe alisema’’ kama mti mubichi unaweza kutendewa hivi itakuwaje kwa mti mkavu?’’ mtu mkavu ni mwanadamu.pia alisema’’ kama mwenye nyumba ametendewa hivi itakuwaje kwa wakaaji wa nyumba?’’

Ujumbe huu umeandaliwa nami M.samlega Willy  mwinjilist na mhubiri,
Kama unashida ya unaweza kunipata kwa mawasiliano hapa chini.
p.o.box 3392
mbeya city-tanzania
email: willyministry@yahoo.com
willhopefoundation@rocketmail.com
simu +255 0762 060641/0713 151874/

5 comments:

  1. JESUS FOR LIFE,TAKE IT OR LEAVE IT...Imani haina kipimo ndio maana haina wizara kwa kila taiga duniani,mwamini Mungu bila kukata tamaa,iwe kwa mgongo au magoti inabidi tuendelee kwenda mbele no matter what...maisha yanifanye yasikufanye ukawambali na Mungu,kila kitu huja kwa sababu....

    Hamjapiga vita hadi kumwaga damu!
    Thanks kwa habari my kaka
    I am the SECOND
    E.M.S
    (MATHEW 11;12)
    mestz15@gmail.com

    ReplyDelete
  2. imenibariki sana mtumishi wa Mungu

    ReplyDelete
  3. Bwana awabariki ,imenifurahisha ile hoja ya petro na papa. hebu nitoe hitimisho lifuatalo ,kamwe huwezi kuokolewa kwa sababu we ni mkatoliki, au pentekoste au seventh adventist au lolote unalolifahamu huko ni kujipa joto kwa moto uliochorwa. mtu anaokolewa sababu amezaliwa kwa Roho wa Mungu na kukubali kutimiza madai ya biblia.Sasa jiite vyovyote kama Hujazaliwa na Roho wa Mungu na unapingana na neno moja tu wala si mengi na maanisha moja la Mungu basi unajaribu kupata joto kwa moto uliochorwa.Na kuna jambo nitakushtua ila usije ukadondoka madhehebu yote tukianzia Romani mpaka ya leo unayoyafahamu ,maana mwanzilishi wa mdhehebu ni Romani yote ni moto uliochorwa ,maana Yesu hakuacha hata moja ya hayo ila wanadamu ndio wameanzisha ,Yesu aliacha Neno lake tu

    ReplyDelete
  4. nina shukuru sana kwa ujumbe huu ambao nilikua niki utafuta sana kati maisha yangu . naitwa imani mbuta arthur niko mkongo drc

    ReplyDelete
  5. Mbona unasema mtume yakobo no ndugu wa Yesu wa Yesu wa kunyonya.Ufafanuzi in muhimu kujua je Yesu alikuwa na ndugu wa kuzaliwa na Maria



    Naomba Ufafanuzi juu ya kwamba Yakobo no ndugu wa Yesu wa kunyonya,je Maria alikuwa na motto mwingine?

    ReplyDelete