WILLY MINISTRY
Wednesday, February 12, 2020
Tuesday, January 21, 2014
MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE KUWA MSHINDI DHIDI YA DHAMBI NA MABAYA YA AINA YOYOTE (IMPORTANT THINGS WHICH YOUR REQUIRED TO DO IN ORDER TO WINER ABOUT SINS)
MAMBO MUHIMU
UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE KUWA MSHINDI DHIDI YA DHAMBI NA MABAYA YA AINA
YOYOTE (IMPORTANT THINGS WHICH YOUR REQUIRED TO DO IN ORDER TO WINER ABOUT SINS) BY WILLY
Ndugu yangu mpendwa
tunakusalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo. Mimi na familia yangu hatujambo
kabisa tunamshukuru Mungu ambaye ameendelea kututunza na kutuvusha mwaka 2012
na kutuingiza mwaka huu wa 2013. Mwaka uliopita kwetu sisi ulikuwa ni mwaka
wenye mafanikio mengi sana. Kwa kweli Bwana alitutnza na kutufanikisha kwenye
mambo mengi sana, kiafya, kiuchumi, kihuduma tumemuona Mungu akitustawisha.
Mwaka jana tumekutana na changamoto nyingi sana pia. Tulimpoteza baba yetu
mpendwa Mzee Seth Mwang'onda. Baba yake mke wangu. Tuliwapoteza ndugu zetu
wengi sana wa karibu. Lakini tunamshukuru Mungu atufarijiaye na kututia
nguvu. Na amini hata wewe mwaka jana Mungu
amekufanikisha sana, na hata ulipokwama mwamini Mungu kukutendea mema mwaka
huu. Pia tunahitaji sana maombi yako mpendwa. Kwani tuna ratiba ndefu sana
mwaka huu, tuombee kwa Mungu ili tufanikiwe sana katika mipango yetu yote. Pia
tunahitaji michango yenu mbalimbali. Unaweza kuingia kwenye eneo la kuchangia
huduma katika tovuti hii na ukapata maelezo. Ebu tusonge mbele tena na
kuziangalia salamu za mwezi huu wa Kwanza kabisa katika mwaka huu wa
2013. Kumbuka Tumekuwa na salamu zenye kichwa
MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE
ILI UPATE KUWA MSHINDI DHIDI YA DHAMBI NA MABAYA YA AINA YOYOTE. (SEHEMU YA
KWANZA). Neno
la Mungu linasema hivi
“Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa ; nayo
yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia;...(Tito 2:11).
Kila mtu aliyeupokea wokovu lazima
ajifunze namna ya kuukataa ubaya na tamaa za kidunia. Ndiyo maana Mungu
imempendeza kuweka neno lake ndani yangu ili kila mtu aliyeokoka ampate
kujifunza mbinu za kuukataa ubaya na tamaa za kidunia. Katika salamu zilizopita
tulianza kuliangalia eneo la MILANGO YA LAANA. Tulianza kuangalia mlango wa
kwanza nao ni ule wa kutokuwaheshimu baba na mama. Mwezi huu tuaangalie mlango
mwingine unaoweza kupitisha laana kwako wewe na hata katika uzao wako.
MLANGO WAPILI:
KUTOKUTOA SADAKA NA UCHOYO
Watu wengi waliookoka hujiuliza swali
hili. Hivi inawezekana mtu aliyeokoka akapatwa na laana? Na wengine hawajui
neno laana maana yake nini. Neno laana maana yake halisi ni nguvu inayozuia
mafanikio ya mtu. Yawe mafanikio ya kiroho, kiafya, kiuchumi, kiakili nk. Sasa
ngoja nijibu swali hilo. Ni ndiyo. Upo uwezekano kabisa ukawa umeokoka kabisaa
lakini ukajikuta umekaliwa na mabaya hayo ya kutokufanikiwa. Moja ya
mlango ambao unawezakupitisha laana katika maisha yako na uzao wako ni huu wa
kutokutii agizo la Mungu la kutoa sadaka na ukarimu.
Watoto wa Mungu wengi hukimbilia
kuomba maombi mengi sana. Wengi hufunga na kuomba sana Mungu awabariki, lakini
wanajikuta kila wanapomaliza maombi yao ndiyo wanazidi kukwama. Wengi hufikria
ni adui amezuia baraka zao. Hufanya maombi ya kukemea roho zinazozuia mafanikio
yao. Lakini wanapomaliza maombi hayo ya kukemea ndipo hukwama zaidi. Wengi
hukimbilia kusema ni majaribu mpendwa. Au utawasikia wakisema ni vita mpendwa!
Sikiliza ndugu yangu ikiwa leo hii wewe hutoi sadaka, na ukitoa unatoa sadaka kilema,
Mungu anakulaani. Angalia maneno haya ya Bwana Mungu jinsi yasemavyo.
“Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake;basi,
kama mimi ni baba yenu heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni Bwana wenu,
kicho changu ki wapi? Bwana wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani,
mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, tumelidharau jina lako kwa jinsi
gani? Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu. Nanyi
mwasema, sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya Bwana
ni kitu cha kudharauliwa. Tena mtoapo sadaka aliyekipofu, si vibaya!na mtoapo
sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya! Haya! Mtolee liwali wako;
je!atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema Bwana wa
majeshi?......... tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani!
Nanyi mmelidharau, asema Bwana wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatika kwa
udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je!
Niikubali hii mikononi mwenu? Asema Bwana. Lakini na alaaniwe mtu mwenye
kudanganya, ambaye katika kundi lake ana mume, akaweka nadhiri, ila amtolea
Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema Bwana wa
majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.” (Malaki 1:6-14).
Ukiyaangalia maneno hayo utagundua
kuwa Mungu amesema wazi kuhusu habari ya kuwalaani watu ambao hawamuheshimu.
Mungu anazungumza na makuhani, hazungumzi na wapagani. Unajua katika agano
jipya kuhani ni mtu gani? Katika Agano Jipya kila mtu ambaye amemwamini Yesu na
kumpokea Mungu amempa nafasi ya kuwa kuhani. Sasa sikiliza kuhani wewe. Mungu
anasema wazi kuwa ikiwa hautoi sadaka kwa uzuri fahamu atakulaani. Mungu
anaikataa sadaka isiyo kamili yeye ameiita sadaka kilema. Kwa lugha nzuri
sadaka dhaifu. Fikiria una shilingi laki moja ya matumizi yako ya kawaida
kabisa, na unapewa nafasi kanisani ya kumtolea Mungu angalia unavyotoa.
Unatoa mia tano. Ungekuwa wewe ndiyo umefanyiwa tendo hilo ungefanya nini? Watu
wengi watoapo sadaka wanatoa vitu dhaifu, ngoja nikupe mfano. Zaka ya shiringi
elfu kumi ni shilingi elfu moja. Wewe unatoa shilingi mia nane. Mungu anakuona
umetoa sadaka kilema. Hiyo ni sadaka isiyokamili
Na anasema kuwa watu hao walisema
jambo hilo limetuchokesha. Ndivyo ilivyo kwa Wakristo wengi. Wanaposikia habari
za sadaka, wengi husema hivyohivyo. Kama wewe ni mtu wa tabia hiyo Mungu
anasema umelaaniwa kwa laana. Angalia maneno haya katika kitabu cha (Malaki
2:1-4).
“Na sasa, enyi makuhani, amri hii yawahusu ninyi. Kama hamtaki
kusikia, na kama hamtaki kuitia moyoni, ili kulitu kuza jina langu. Asema Bwana
wa majeshi, basi nitawapelekeeni laana. Nami nitazilaani baraka zenu; naama
nimekwisha kuzilaani. Kwa sababu hamyatii haya moyoni. Angalieni, nitaikemea
mbegu kwa ajili yenu, nami nitapaka nyuso zenu mavi, naam mavi ya sadaka zenu;
nanyi mtaondolewa pamoja nayo.”
Mungu anasema wazi kuwa ikiwa
hatutayatia moyoni maagizo yake ya kutoa sadaka, basi atakachokifanya ni
kutulaani. Anasema atapaka mavi katika sura yako. Ebu fikiria ni Wakristo
wangapi ambao hawatoi sadaka vizuri na leo hii wanatafuta mpenyo wa kupenya
katika suala la mafanikio yao lakini wamekwama? Ni wengi mno. Sikiliza mpendwa
leo hii jambo baya sana la kutokufanikiwa kiuchumi limewakalia watu wengi sana,
kisa ni laana inayotokana na kutokutoa sadaka, watu wengi hawatoi sadaka ila
wanataka baraka. Hata watumishi wa Mungu wengi wamejikuta wamekwama kisa ni
hikihiki cha kutokutoa sadaka. Sikiliza mtumishi unatakiwa ujifunze kumtolea
Mungu sadaka. Neno la Mungu linatufundisha kuwa Mungu aliwaagiza Walawi na hata
Makuhani wahakikishe wanatoa sadaka. Angalia maneno haya ya Bwana jinsi
yasemavyo.
“Bwana akanena na Musa na kumwambia, matoleo ya Haruni na wanawe
watakayo mtolea Bwana , katika siku atakayotiwa mafuta, ni haya;.....” (Mambo
ya Walawi 6:19-23).Angalia na mistari hii. “Kisha Bwana akanena na Musa na
kumwambia. Tena utanena na Walawi na kuwaambia hapo mtakapoitwaa
zaka mkononi mwa wana wa Israeli, niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa
urithi wenu, ndipo mtakaposogeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana
katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka. Na sadaka yenu ya kuinuliwa itahesabiwa
kwenu kama ndiyo nafaka ya sakafu ya kupuria, na kama kujaa kwake kinu cha
kushindikia zabibu. Hivyo ninyi nanyi mtasogeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana
katika zaka zenu zote. Mpokeazo mikononi mwa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni
kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana.....”(Hesabu 18:25-32).
Mungu anatufundisha kupitia maneno
hayo wazi kuwa hata watumishi walitakiwa wajifunze kutoa sadaka.
Kwa nini leo hii watumishi wengi ni
masikini sana? Jibu lake ni hili, angalia utoaji wao wa sadaka. ndipo utakapo
ona kinachowazuia wasifanikiwe kiuchumi. Watumishi walitakiwa kutoa zaka
na matoleo mbalimbali ili na wao wapate kubarikiwa na Bwana. Lskini watumishi
wengi hawatoi sadaka. Kutokana na kutotii maagizo hayo ya Bwana katika kona hii
ya kutoa sadaka, ndio maana utaona watoto wa Mungu wengi hawafanikiwi kiroho,
kiafya, kiuchumi nk.
Ndugu jifunze kuwa mkalimu, ndipo
utapoepukana na jambo baya la laana. Sikiliza Bwana Yesu anatufundisha wazi
kuwa lazima tuwape watu vitu ndipo nasi tutakapopewa vitu. Angalia maneno ya
Bwana Yesu Kristo.
“Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa,
na kusukwa-sukwa hata kumwagika. Ndicho watu watakachowapa vifuanimwenu. Kwa
kuwa kipimo kilekile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.” (Luka6:38).
Kama unataka leo mafanikio lazima
ujifunze kuwa mkarimu kwa watu na kwa Mungu pia. Angalia namna watoto wa Mungu
wengi tulivyo. Utaona tumejaa ubinafsi mwingi sana. Mungu atusamehe na
kutuondolea laana. Fikiria namna watu wengi wanavyotaka kupewa vitu mbalimbali
kwa wingi, wakati wao hawataki kutoa vitu kwa watu. Hivyo ndivyo tulivyo.
Badilika mpendwa ili utoke kwenye laana iliyokukalia. Sikiliza mpendwa Bwana
anakupenda sana ndiyo maana leo hii ana kupatia ujumbe huu mzuri ili
ubadilike kutoka kwenye tabia hiyo mbaya ya uchoyo. Siku moja Mungu
alinifundisha faida ya ukalimu. Ona mfano huu wa namna Mungu alivyompa Ibrahimu
mtoto. Neno la Mungu linasema, Ibrahimu aliwakaribisha nyumbani kwake watu
watatu. Walipokaa hapo ndani na kula chakula, ndipo Bwana alipomwambia Ibrahimu
kuwa Sara atakuwa na mtoto wakati kama huo mwakani. Fikiria kama Ibrahimu
asingewapokea wageni hao ambao walikuwa ni malaika wawili na Bwana
Mungu mwenywe.
Na amini kuwa asingelikuwa mkalimu
muujiza wake ungelimpita hivi hivi. Soma Kitabu chote cha (Mwanzo18:1-15)
utaiona habari hiyo nzuri ninayokuambia. Sehemu nyingine neno la Mungu linatupa
akili likisema hivi.
“Msisahau kuwafadhili wageni maana kwa njia hii
wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.” (Waebrania13:2)
Fikiria leo hii umemkilimu malaika
wa Bwana alipokuja nyumbani kwako, unafikiri Mungu atakufanyia nini? Na amini
Mungu atakubariki sana. Ebu tumalizie salamu hizi za mwezi huu mpya wa kwanza
kabisa kwa mwaka huu wa 2013 kwa kujifunza kuwa watoto wakalimu na watoaji
sadaka njema kwa Mungu ili tufunguliwe kutoka katika mkandamizo wa laana.
Nakushauri jipange moyoni mwako kwa kujiwekea malengo maalumu kwa kujitoa zaidi
katika kuhakikisha unafadhiri kazi ya Mungu kwa mali zako, jiwekee malengo ya
kuwatunza watumishi wa Mungu na hata kuwafadhiri watu ili Mungu akufungulie
mlango wa baraka nyingi kwa mwaka huu wa 2013. Mungu akubariki sana
BY EVENGEILIST
WILLY M. SAMLEGA
Thursday, January 9, 2014
KWA NINI NINAPASWA KUOKOKA (WHY SHOULD I REVEVE SALVAVATION?) BY WILLY
Kwa nini ninapaswa kuokoka?
Inakupasa
ndugu kuupokea wokovu kwa sababu ndio mapenzi ya Mungu, Watu wengi sana
wamezoea kusema hayakuwa mapenzi ya Mungu, au wengine kuomba hivi “ Mapenzi ya
Mungu yafanyike” tena wengi wameizoelea ile sala kuu kila waendapo kwenye
makusanyiko mbalimbali huisema ile sala kuu na katika hiyo sala kuu kuna eneo
ambalo wanaomba wakisema “Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko
mbinguni” (MT 6:10). Ninaamini hata wewe sla hii unaifahamu na
unamuomba Mungu kila mara mapenzi yake yatimizwe hapa duniani au kwako,kwa
jamaa zako na ndugu zako, Lkini nikikuuliza swali je! Unayajua mapenzi hayo ya
Mungu amabayo unataka yatimizwe hapa duniani! Bahati mbaya watu wengi hawayajui
hayo mapenzi ya Mungu.
Ukisoma
maandiko matakatifu utaona kuwa miongoni mwa hayo mapenzi ya Mungu, hili la
kila MTU aokolewe au AOKOKE! Ebu sikia maneno haya ya semavyo “Hili ni
zuri,nalo la kubarika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote
waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu Mungu ni mmoja na
mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja,mwanadamu Kristo Yesu, ambaye
alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira
yake”. (1Timotheo 2:3-6) Kama kuna jambo ambalo limepata kibari
au limekubarika na Bwana Mungu na yeye analiona ni zuri, hili la watu
waokolewe, na mtu huyo ni wewe! Kwa nini wewe uokoke? Jibu mojawapo
ni hili una kuwa unayatimiza mapenzi ya Mungu. Mungu anataka wewe uokolewe na
Mwokozi ni mmoja naye ni Yesu Kristo.
Usipo
okoka fahamu una kuwa kinyume na mapenzi ya Mungu, na mtu yeyote yule asiye ya
tenda yaliyo mapenzi ya Mungu hata upata uzima wa milele, kwa hiyo na kushauri
leo kubali mapenzi ya Mungu ya timizwe kwako, au kwa ndugu na jamaa zako. Watu
wengi wanayazuia mapenzi ya Mungu yasifanyike kwao,au kwa watu wengine, lakini
kwa bahati mbaya huwa hawajui kuwa wao ndio kizuizi cha mapenzi ya Mungu
kutimizwa kwao au kwa watu wengine, unaweza kusema una maana gani?
Sikiliza,
unapokataa au unapokataza watu wengine wasiupokee wokovu
unakuwa unayazuia mapenzi ya Mungu, na jambo hio ni dhambi. Watu wengine
huwazui watu wasiokoke, wewe unapolizuia jambo hilo kwa kulikataza,
unakuwa kinyume na mapenzi ya Mungu, kumbuka Mungu anasema jambo hilo yeye
analikubali,na ni zuri kwake. “Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za
za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe....” (1Timotheo
2:3-6), Kwa ufupi unatakiwa leo ujue kuwa unapaswa kuupokea wokovu kwa
sababu ni mapenzi ya Mungu, si mapenzi ya watu fulani au ya dhehebu Fulani,
wokovu ni mapezi ya Mungu kwa kila mtu, Swali langu kwako, je! Umeokoka?
Kama bado fahamu unayazuia mapenzi ya Mungu nakushauri yaruhusu leo
mapenzi ya Mungu yatimizwe kwako, kwa kuupokea huo wokovu.
BY WILLY M.SAMLEGA
SALAM MAALUM ( SPECIAL GREATINGS) BY WILLY
SALAM
MAALUM ( SPECIAL GRETINGS)
Ebu
Soma Maneno Haya."Akanena mfano huu; mtu mmoja alikuwa mtini umepandwa
katika shamba lake la mizabibu, akaenda akitafuta matunda juu yake
asipate.akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii
naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu nisipate kitu; uukate mbona hata
nchi unaiharibu? Akajibu akamwambia Bwana uuche mwaka huu nao, hata niupalilie,
niutie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate."(Luka
13:6-9).
Umeyaona
Maneno hayo? Mungu amekupa mwaka huu mpya anasababu nzuri tu. ukiyaangalia
maneno hayo unagundua kuwa ikiwa mimi na wewe hatumzalii Mungu matunda basi
huwa na tabia ya kutukata. Hata Kwenye kitabu cha Yohana15:1-5 anazungumzia
jambo hilihili. Hapo anasema. Kila tawi lililo ndani yake ambalo halizai
matunda hulikata. Fikiria tawi lililo ndani yake kama halizai matunda Yesu
analikata. Kumbuka si yale matawi yaliyo nje yake! Anasema yaliyondani yake!
Wewe leo hii umepewa nafasi ya kuuona mwaka huu inawezekana unapaliliwa na
umewekewa samadi yaani mbolea ili uanze kumzalia Mungu Matunda. Na kama
ulimzalia mwaka uliopita basi mwaka huu uzidushe matunda ili USIKATWE!
Matunda
nini? Matunda ni matokeo! Au tabia. Ebu angalia mwaka uliopita ulikuwa na tabia
gani? Kama ulikuwa na tabia mbaya basi badilika mwaka huu. Neno la Mungu
limeyataja matunda yapatayo manne.
1.
2.
Tunda la kazi. (Wafilipi 2:
21-24).
2. Tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23).
3. Tunda la midomo iungamayo jina la Bwana (Waebrania13:15)
4. Tunda la haki ( Yakobo3:18).
2. Tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23).
3. Tunda la midomo iungamayo jina la Bwana (Waebrania13:15)
4. Tunda la haki ( Yakobo3:18).
Hayo
ndiyo matunda Mungu anataka umzalie sana.
Tunda
la kazi: kuna aina mbili za kazi. Kazi ya mikono. Na kazi ya kumtumikia
Mungu. Kila Mkristi anawajibu wa kuujenga Ufalme wa Mungu. Kama
kuhuburi injili kufundisha nk. Unaweza kutumika kwa kuomba. Ona maombi
yako ya mwaka jana yalikuwaje? Uliwaombea watumishi kwa kiwango gani?
Ulitoa mali zako kwa kiwango gani ili kazi za Mungu zitendeke? Wewe
mwenyewe jipime. Kama hukufanya kwa uzuri badilika mwaka huu.
Tunda
la midomo: Lazima uhakikishe midomo yako aisemi mambo madhaifu yaani
usikiri udhaufu. Usitukane usiseme uongo nk. Swali langu kwako ni hili ni
kiwango gani ulikuwa nacho mwaka uliopita cha kumtukuza Yesu Kwa kupitia
kinywa chako? Ulimlaumu Mara ngapi na ulimsifia mara ngapi? Mwaja huu badilika
Tunda
la Roho: tabia yako ilkoje? Unaupendo kwa watu kwa kiwango gani? Je! Moyoni
mwako umeifadhi huzuni au furaha? Je! Ni mtu wa uliyekata tamaa au umejaa
uvumilivu? Wewe ni mtu wa namna gani? Ni mpole wewe au ni mkatili? Jipime, kama
mwaka jana ulikuwa na tabia mbaya mwaka huu badilika
Tunda
la haki: je! Wewe ni mtu wa Haki? Unawapa watu wote haki zao zilizo mkononi
mwako? Je! Una amani na watu wote? Tunda la haki linazaa amani na kila mtu
angalia maneno haya ". Na kazi haki itakuwa amani; na mazao ya haki
yatakuwa ni utulivu na matumaini daima"
(Isaya 32:18).
Je!
Wewe ukoje! Unamatumaini au umepoteza matumaini? je! Wewe ni mtulivu? Kwa
kiasi gani? Ukiudhiwa unatukua au ndiyo unapoteza utulivu na kulipa kisasi.
Ndugu
ebu jipime matunda yako uliomzalia Bwana yakoje. Kama hayaja kaa sawa basi
rekebisha mwaka huu. Kama tako vizuri basi usijiruhusu kuludi nyuma songa
mbele.
Nakutakia
baraka na amani tele katika Mwaka huu mpya. Yesu awe nawe na atukuzwe kwa
kupitia wewe. Barikiwa!!!!
MAISHA BAADA YA WOKOVU /LIFE AFTER BEING BORN AGAIN
Maisha baada ya kuokoka...
Maisha baada ya wokovu - Je yanipasa kuishi maisha gani?
Ikiwa umepata wokovu, basi
yapo mambo ambayo inakupasha kuyafanya na kuyaishi. Jifunze juu ya mambo haya.
Mambo ya msingi
yakupasayo kuyafanya baada ya kuokoka
Ndugu yangu baada ya kuokoka
tu, kuna swali na amini liko ndani ya moyo wako, unajiuliza, sasa leo hii
nimeokoka nifanyenini sasa? Ni kweli ikiwa umeokoka kuna mambo
muhimu ambayo unatakiwa uanze kuyafanya, yapo mambo mengi sana,lakini ebu
nikupe haya mambo ya msingi ambayo unapaswa kuyafanya.
Jambo la
kwanza
===============================================
Jambo la kwanza
ambalo Mungu anataka kuliona kwako likitendeka baada ya kuokoka, ni
kukuona ukiukulia Wokovu. “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini
maziwa ya akili yasiyo ghoshiwa,ila kwa hayo mpate kuukulia wokovu;” (1PETRO
2:2)
Baada ya wewe kuhamishwa
kutoka katika ufalme wa giza na kuingizwa katika ufalme wa Nuru, yaani chini ya
utawala mpya ambao unataratibu tofauti na ule utawala wa kwanza ambao
inawezekana umeishi chini ya utawala huo kwa muda wa miaka mingi, Mungu anataka
akuone sasa ukianza kuyajua mambo mapya yaliyoko katika utawala
wake, anaposema kuukulia wokovu, maana yake kubwa ni
kuzidi kuyajua mapenzi yake Mungu, Uzidi kujua kwa upana
upendo wake kwako, uzidi kujua Uwezo wake ulivyo mkuu na nguvu zake zilivyo,
uzidi kujua ni nini umekusudiwa ukipate baada ya kuingia katika Ufalme wa Nuru,
ona maneno haya yasemavyo, “Kwa sababu hiyo mimi nami,tangu nilipopata
habari za imani yenu katika Bwana Yesu,na pendo lenu kwa watakatifu wote,siachi
kutoa shukrani kwa ajiri yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu, Mungu wa Bwana
wetu Yesu Kristo,Baba wa utukufu,awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika
kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, MJUE tumaini la mwito wake jinsi
ulivyo; na UTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHI WAKE KATIKA WATAKATIFU JINSI ULIVYO;
kwa kadili ya utendaji wa nguvu za uweza wake;…” (WAEFESO 1: 15-19)
Neno la Mungu linatufundisha
hapo kuwa Mungu anataka wewe na mimi baada ya kuokoka tu kwa njia ya
imani, tuanze kuyajua hayo mambo aliyoyataja Mtume Paulo na mengine
mengi, anataka ujue tumaini la wito wake jinsi ulivyo, Mungu amekuita baada ya
kukita amekukusudia nini? Anataka ujue baada ya kuokoka nini unachotakiwa
ukitalajie kutoka kwake, ujue baraka zako au haki zako ambazo Mungu amewa
ahidia kuwapa wale wote walio upokea huo wokovu, kwa mfano Baada ya wewe
kuokoka, Kuna kuna vitu ambavyo Mungu anakupa, anataka uvijue, angalia maneno
haya “Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono wangu wa
kuume,hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je! Hao wote si roho
watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale wataourithi wokovu!” (EBR 1: 13-14)
Neno la Mungu hapo
linatufundisha kuwa moja ya baraka amabazo walioupokea wokovu wanazipokea ni
hizi za kupewa wahudumu wa kuwahudumia, na wahudumu hao ni
malaika. Mtume Paulo alijua wazi kuwa kunamambo mengi ambayo Mungu
ameyakusudia kuwapa watu wote watakao urithi wokovu, akaamua kuwaombea hao
watu ili Mungu awasaidie kuyajua hayo yote, akawaombea hao ndugu
waliompokea Yesu kama Bwana na mwokozi wao wapewe Roho ya ufunuo wa
kumjua Mungu, pia akawaombea wapate ufahamu rohoni mwao wa kujua utajiri waliopewa
na Mungu baada ya kuokoka, pia macho yao ya ndani yaone kila kitu ambacho Mungu
anacho na amekiweka kwa ajiri ya watu wale walioamua kumpa Yesu maisha
yao.
Na amini umeelewa maana ya
kuukulia wokovu sasa, Sikia tena,unapozidi kujua ndipo unapozidi
kukua, au kwa lugha nzuri ndipo ufahamu wako wa kumjua Mungu unapokuwa mkubwa,
na hilo ndilo kusudi la Mungu kwako, anataka akukuze ufahamu wako katika kumjua
yeye na pia uyajue mapenzi yake kwa upana zaidi, angalia maneno yake haya ya semavyo
kuhusu jambo hili “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile
tuliposikia, hatuachi.kufanya maombi na dua kwa ajiri yenu,ili mjazwe maarifa
ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni” (WAKOLOSAI 1:9.) Mungu
anataka wewe ndugu upate kujazwa maarifa,hekima na ufahamu wa rohoni, mambo ya
rohoni ni mambo ya Kimungu, anataka ujazwe ufahamu wa mambo ya kimungu, Hiyo
ndiyo maana ya kuukulia wokovu.
Namna ya kufanya
Ili upate kukua au kuanza
kuyajua mambo hayo yote, unatakiwa uanze kuyanywa maziwa
yasiyoghoshiwa. Neno hilo lina maana maziwa yasiyochanganywa
na maji, mtoto mchanga azaliwapo, huwa hapewi chakula kigumu,
hunyonya maziwa ya mama yake, na kama akipewa maziwa ya ng’ombe au mbuzi, ni
lazima maziwa hayo yachanganywe na maji kidogo, hata wewe ili leo
hii uanze kuukulia wokovu inatakiwa uanze kunywa maziwa yasiyo changanywa na
maji, “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili
yasiyoghoshiwa, ila kwa hayo mpate kuukulia wokovu;” (1PETRO 2:2) Maziwa
hayo Neno la Mungu linayaita “maziwa ya akili”, au maziwa ya
ufahamu, unaweza ukawa na swali maziwa hayo nini? Maziwa hayo ni
Neno la Mungu, angalia maneno haya yasemavyo “ Ambaye tuna maneno mengi
ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa
kusikia. Kwa maana,iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita)
mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi
mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu kwa maana kila mtu atumiaye
maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni motto mchanga. lakini chakula
kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao kwa kutumiwa zimezoezwa kupambanua
mema na mabaya. ” (EBR 5:11-14)
Ukisoma maneno hayo
kwa kutulia utagundua wazi kuwa, Biblia inapozungumzia hapo kuhusu
maziwa inataja wazi kuwa maziwa ni Neno la Mungu, Kwa maana hiyo
kama unataka kuukulia wokovu unatakiwa uhakikishe unalitafuta neno la Mungu
iliutoke katika hali ya utoto na ukue. Hao ndugu walikuwa watoto kwa sababu
walikuwa wavivu wa kulisikia neno la Mungu, “ Ambaye tuna maneno mengi
ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa
kusikia.” (EBR 5:11) Kitu kilichopelekea hao ndugu
kukaa katika hali ya utoto kwa muda mrefu ni uvuvi waliokuwa nao wa kulisikia
neno la Mungu, Kama unataka kuukulia wokovu unatakiwa uhakikishe
unaondoa uvivu wa kulisikia neno la Mungu, neno la Mungu tunaweza kulisikia kwa
namna nyingi sana, Kwa kulisoma, Fahamu unaposoma unasikia, weka bidii kusoma
Biblia, kusoma vitabu mbalimbali ambavyo waalimu wa neno la Mungu wameviandika,
pitia tovuti (website) mbalimbali za watumishi wa Mungu, soma waliyoyafundisha
nenda kayahakikishe kwenye Biblia yako kama ni sahihi. Pia unaweza
kusikia mafundisho kwa kupitia semina,mikutano, ibadani kwenu, hata kwa kununua
kanda za mafundisho ya neno la Mungu, cd.au vcd ama dvd nk. Ukiweka bidii
katika kusikia fahamu hata imani yako kwa Mungu itakuwa kubwa sana, pia ufahamu
wako wa Mambo ya Mungu utaongezeka siku hata siku. Ndani ya neno la Mungu huko
ndiko kuna maarifa na ufahamu wa kumjua Mungu na kumcha. Sikiliza haya maneno
ya Mungu yasemavyo“ Mwanangu. Kama ukiyakubari maneno yangu na kuyaweka
akiba maagizo yangu; hata ukatega sikio lako kusikia hekima, ukaelekeza moyo
wako upate kufahamu; naam ukiita busara na kupaza sauti yako upate ufahamu;
ukiutafuta kama fedha, na kuutafuta kama hazina iliyositirika; ndipo
utakapofahamu kumcha Bwana, na kupata kumjua Mungu.” (MITHALI 2: 1-5)
Ili
leo hii upate ufahamu, upate kujua kumcha Mungu, lazima uweke bidii ya
kulitafuta neno la Mungu kama vile unavyotafuta fedha, kama unabidii kubwa ya
kutafuta fedha bidii hiyo hiyo unafundishwa uiweke katika kulitafuta neno la
Mungu, ndani ya neno la Mungu huko ndiko kuna maarifa yote, ili leo hii upate
kuishinda dhambi yapo maarifa ndani ya neno la Mungu, ili leo hii upate
kubarikiwa, maarifa ya kubarikiwa yapo ndani ya neno la Mungu, neno la Mungu
ndio dila ya maisha yote atakayo Mungu uyaishi ukiwa hapa duniani, Mungu
ameweka siri zake humo ndani ya neno lake. Ili uendelee kuokolewa kila siku
maarifa yake yamo ndani ya hilo neno la Mungu, inawezekana ukawa na swali hili
ikiwa nimekosea baada ya kuokoka ninatakiwa nifanyenini?, Sikia maarifa hayo
yamo ndani ya neno la Mungu sikia neno lisemavyo “ Watoto wangu wadogo,
nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye
mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi
zetu; wala si kwa dhambi zetu tu,bali na kwa dhambi za ulimwengu wote” (1YOHANA
2:1-2) Weka bidii ya kulisoma neno la Mungu,na kulisikia hapo
ndipo utakapo ukulia wokovu. Naamini umeelewa jambo la Kwanza.
Jambo
la pili
===============================================
NI
KUOMBA AU (KUZUNGUMZA NA MUNGU)
Jambo la pili muhimu ambalo
unatakiwa ulifanye ni kuomba. Nini maana ya kuomba? Kuomba ni kuzungumza au
kushirikiana na Mungu, Mungu anataka kushirikiana na wewe, Kumbuka ulipo okoka
alilejeza ushirikiano kati yake na wewe, kwa hiyo anataka kuudumisha ushirika
huo, na ushirika huo utaudumisha kwa kupitia maombi, Neno la Mungu linasema
hivi “Haya njooni tusemezane,asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu
sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera,zitakuwa
kama sufu” (ISAYA 1: 18). Mungu anataka kusema nawe, na amekupa kibali
cha wewe kwenda kuzungumza naye, ameamua kukusamehe, na baada ya
kukusamehe,amekupa nafasi ya kusema naye, tunasema na Mungu kwa njia ya
maombi.
Baada ya kumpokea Yesu
fahamu yuko ndani yako, hayupo mbali na wewe yuko karibu, anachotaka ni wewe
kumshirikisha kila jambo, ukiwa unauhitaji fulani anataka umwambie
akusaidie, angalia maneno haya ya Mungu yanavyotufundisha, “
Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini, upole wenu na ujulikane
na watu wote. Bwana yu karibu. msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila
neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na
zijulikane na Mungu” (WAFILIPI 4:4-7)
Mungu anataka
umshirikishe kila unacho hitaji, hapendi kukuona wewe ukijisumbua peke yako,
anataka ushirikane naye umweleze kila kitu, usimfiche ikiwa umekwama katika
kona fulani mweleze nk. Hata ukikosea omba maombi ya kuomba msamaha,
atakusamehe, ikiwa unaumwa omba uponyaji atakusaidia, ikiwa unashida yoyote ile
mwambie, atakusikia kwa kuwa hayupo mbali nawe, kumbuka yupo karibu sana na wewe
kuliko vile unavyo fikiri. Unaweza kuwaza moyoni mwako kuwa mimi sijui kuomba,
sikiliza hakuna anaejua kuomba. Neno la Mungu lina sema hivi, “Kadharika
Roho naye hutusaidia udhaifu wetu,kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo;
lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, naye
aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama
apendavyo Mungu.” (WARUMI 8: 26-27)
Mimi na wewe hatujui
kuomba. Neno la Mungu linasema wazi hapo, wewe anza kuomba tu,
usiogope kuwa utakosea, ondoa wazo kuwa Mungu anawasikia watu Fulani tu, Mungu
anamsikia kila mtu aliye na imani kwake, na ambaye hamfichi dhambi zake,
kumbuka anasema njooni tusemezane, amekuahidi kukusafisha dhambi
zako zote, hata kama ni nyekundu sanaa, anachotaka ni hiki, usimfiche maovu
yako, ziungame dhambi zako zote mbele zake, atakusamehe,ndipo umuombe, na
ukimwomba atakupa hicho umwombacho, kama unataka kuukulia wokovu,
weka bidii katika eneo hili la kuomba. Kinachotakiwa ukifanye kwenye
maombi yako omba kwa Jina la Yesu Kristo. Usisahau kulitumia jina hili katika
maombi yako, ili maombi yako yashughulikiwe mbinguni, lazima uyagonge muhuli wa
jina la Yesu Kristo. Bwana Yesu anatufundisha kuhusu habari za maombi
anasisitiza sana kuhusu jambo hili la kuomba, na anapo tufundisha kuomba
anatutaka tunalitumia jina la Yesu katika maombi yetu. “ Tena
siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin,
nawaambia,mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu. Hata
sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni nayi mtapata; furaha yenu iwe
timilifu” (YOHANA 16:23-24)
Jifunze kulitumia jina la
Yesu katika maombi yako, pia jifunze kuwasamehe watu wote waliokukosea kabla
hujaingia kwenye maombi. Neno la Mungu lina sema hivi “ Nanyi kila msimamapo
na kusali,sameheni mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni
awasamehe ninyi makosa yenu. (Lakini kama ninyi hamsamehe,wala Baba
yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu)”
(MARKO
11: 25-26). Jifunze kuwasamehe watu wote waliokukosea kabla
haujaingia kuomba, kwa kufanya hivyo utajikuta unafanikiwa sana katika eneo
hili la kushirikiana na Mungu kwa njia ya maombi. Hili ni jambo Muhimu
katika habari za kuukulia wokovu ulioupokea.
Jambo
la tatu
===============================================
Jambo la tatu ni hili,
waambie watu wegine kuwa umeokoka. Sikiliza ikiwa leo hii unataka Mungu azidi
kukukuza katika wokovu unatakiwa ujifunze kumkiri Yesu kwa kupitia kinywa chako
kama Bwana na mwokozi wako, sikiliza maneno haya yanavyotufundisha. “Kwa sababu
ukimiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa bni Bwana, na kuamini moyoni kuwa Mungu
alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu uamini hata kupata
haki,na kwakinywa hukiri hata kupata wokovu” (WARUMI 10:9-10). Maneno
hayo ya Bwana yanatupa maarifa makubwa sana, unatakiwa uamini moyoni mwako na
pia uanatakiwa ukiseme kile ulichokiamini anasema wazi kuwa ili uupate wokovu
inakusapasa ujifunze kuamini moyoni kuwa Yesu ndiye Bwan mwokozi wako, na pia
ukiri au useme kwa kinywa chako kuwa Yesu ndiye Bwana na mwokozi
wako, ikiwa leo hii umempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wako
usiogope kuwambia watu wengine kuwa UMEOKOKA!. Ukifanya hivyo ndipo unapoumbiwa
wokovu kila siku, kwanini useme? Sikiliza Mungu anaumba matunda ya kinywa
chako. “Mimi nayaumba matunda ya midomo” (ISAYA 57:19A).
Mungu ana tabia ya kuyaumba
yale uyasemayo, sasa ikiwa leo hii utaanza kukiri au kusema Yesu ameniokoa,
ndipo Mungu atapo umba wokovu kwako! Umeona hilo jambo la tatu lilivyo muhimu?
Kama leo hii hutaki kwenda mautini, lazima ujifunze kuumba pamoja na
Mungu wokovu wa kukutoa mautini. Unaweza kujiuliza nitaumbaje pamoja na Mungu?
Sikiliza Mungu anayaumba yale uyasemayo, ukisema umeokoka kutoka
mautini na Yesu ndiye mwokozi wako, fahamu ndipo utakuwa unaumba wokovu huo pamoja
na Mungu, kwa kuwa Mungu anaumba yale tuya semayo, ebu angali maneno haya
yasemavyo. “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao wa upendao
watakula matunda yake.” (MITHALI 18 : 21). Kuna nguvu kubwa sana ya
uumbaji kupitia maneno uyasemayo, neno la Mungu hapo linasema mauti na uzima
huwa katika uwezo wa ulimi. Yaani kile unachokisema ndicho kitakacho kupa Uzima
au mauti, iwapo utaanza kusema kuwa umeokoka, basi fahamu ndipo utakapokuwa
unaumba uzima katika maisha yako . Basi ndugu yangu mpendwa
ikiwa umeokoka usisite kusema kwa watu kuwa umeokoka! Hapo utakuwa
unaukulia wokovu.
Na amini kwa sehemu
umefahamu ni mambo gani muhimu unayotakiwa uyafanye baada ya kuokoka, ya fanyie
kazi na ndipo utakapo ukulia wokovu, Mungu Yesu Kristo akubariki sana.
by willy m.samlega
Monday, December 23, 2013
JUSES WAS BORN IN BETHELEHEUM ,HE WANT TO BE BORN IN YOUR HEART THIS CHRISTMAS
LONG TIME AGO JUSES CHRIST WAS BORN MANY PROPHET THEIR PROCLAMED ABOUT HIS BIRTH, LOOK AT LUKE 2:1.....................
Dr LUKE IS WRITE ABOUT THE BIRTH OF OUR LORD JUSES CHRIST, 25 DECEMBER EVERY YEAR THE WOURLD IS CELEBRATIG THE BIRTH OF JUSES CHRIST, THE MATER HERE IS NOT TO CELEBRATE IS TO ASK JUSES TO TAKE PLACE IN YOUR LIFE(HEART).
THE BIBLE EXPLAIN THAT MARY AND JOSEPH THEIR FAILED TO GET A ROOM AT GUEST HOUSE, BECAUSE MANY VISTORS AT BETHELEHEUM, THEIR DICED TO FIND APLACE WHERE MARYCAN HAVE A PLACE IN ORDER TO HAVE A CHILD, SHE WAS A PREGNANT.
THIS WEEK JUSES LOOKING A PLACE IN ORDER HIM TO BE BORN IN YOUR HEART.
BY EVENGELIST
WILLY.
Dr LUKE IS WRITE ABOUT THE BIRTH OF OUR LORD JUSES CHRIST, 25 DECEMBER EVERY YEAR THE WOURLD IS CELEBRATIG THE BIRTH OF JUSES CHRIST, THE MATER HERE IS NOT TO CELEBRATE IS TO ASK JUSES TO TAKE PLACE IN YOUR LIFE(HEART).
THE BIBLE EXPLAIN THAT MARY AND JOSEPH THEIR FAILED TO GET A ROOM AT GUEST HOUSE, BECAUSE MANY VISTORS AT BETHELEHEUM, THEIR DICED TO FIND APLACE WHERE MARYCAN HAVE A PLACE IN ORDER TO HAVE A CHILD, SHE WAS A PREGNANT.
THIS WEEK JUSES LOOKING A PLACE IN ORDER HIM TO BE BORN IN YOUR HEART.
BY EVENGELIST
WILLY.
Monday, December 9, 2013
LIFE OF APOSTELS AND THEIR DEATH/ MAISHA YA MITUME NA VIFO VYAO
MAISHA NA VIFO VYA MITUME WA BWANA YESU KIRISTO.
YESU ALISEMA MTU AKITAKA KUMFUATA SHARITI AJIKANE MWENYEWE NA KUUBEBA MSALABA WAKE NDIPO AMFUATE:MATHAYO 16:24 SOMA WAFILIPI 1:29 1PETRO 4;14
MTUME PETRO.
Mtume Petro a lipata mateso makalili aliya pata kwa kusulubiwa kichwa chini miguu juu, hii ni adhabu aliyo I chagua yeye baada ya kushitakiwa kwa ajili ya kumhubili bwana yesu. Hakutaka kusulibiwa kama yesu kiristo.
MTUME YOHANA (YOHANA NTAKATIFU)
Mtume huyu alipendwa sana na bwana yesu kwa mjibu wa bilbilia na vitabu mbalimbali kama histoaria ya kanisa, bibilia ya mafunzo ya uzima tele, pia comentally ya bibilia, bible dictionary,
Ni mtume pake yake aliye kufa kifo cha kawaida, ila alipitia majilbio kadha wa kadha ya kumuua,
>mtume huyu aliwekwa kwenye pipa la mafuta yanayo chemuka lakini alitoka hai,
>mtume huyu alikatwa kichwa bila mafanikio ya watesaji bila kukatika shingo yake
>Alifungwa nyasi mwili mzima na kuchomwa moto, nyasi ziliungua lakini yeye na nguzo zake hakuungua
>Alipigwa mawe mpaka walipo lizika na kuzani amekufa lakini aliinuka na kuendelea na shughuli zake kama kawaida
>kaisari Domatian aliamua kumtupa katika kisiwa cha patimo, ili afe huko kisiwa kilikuwa kimejaa barafu na baridi lakini hata hivyo mtume yohana hakufa badala yake akapata ufunuo wa kitabu cha ufunuo wa yohona. Jambo lamaana ni kwamba mtume yohana akiwa patmo alipwe ufunuo,wakati maadui wa injili walio dhani baridi na njaa vitamuua mtume yohona matokeo yake ni kupata ufunuo wa mbiguni. Inasemekana mtume yohana baada ya kuhubili injili huko efeso alikufa kifo cha kawaida tu huko efeso.
MTUME YAKOBO
Mtume yakobo nimutume wa wanza kuuwawa na ndiye mtume pekee ambaye habari za kifo chake zimeandikwa katika kitambu cha matendo ya mitume.
>mtume huyu alishitakiwa kwa mashitaka ya uongo kisha wakampeleka mahali pa kukatwa kichwa kwa upanga. Jambo la kutia moyo katika historia hiyo ni pale Yule mtu laliy jitolea au aliye pedekezwa na heredo kutoa mashitaka ya uongo. Aliamua kumsindikiza mtume yakobo akiwa anakwenda kuuwawa baada ya kuona muonekano wa mtume yakobo ni tofauti na vile alivyo tarajia.kwani alitalajia kuwa angekuwa mnyonge, mwenye hofu na mashaka lakini matokeo yake mtume yakobo akawa mwenye furaha kuu akiimba nyimbo za kumsifu mungu.yule mtoa mashitaka ya uongo alipo ona hayo alishikwa na hofu kuu na kuamini kuwa kweli mungu yu pamoja na mtume yakobo.wakati wa kuuwawa kwake,yakobo aliona uso wake uking’aa kwa furaha kuu ndipo naye akaamuua kumpokea bwana na kutangaza kuwa naye ameokoka . wote wawill walikatwa vichwa siku moja kwa upanga ule ule.
MTUME MATHAYO
Mtume huyu mathayo ni Yule ambaye alikuwa mtoza ushurumaliko 2:14 mthatyo 9:9 mtume alihubiri maeneo mbalimbali,kama jelusalem, Ethiopia, iran,
> mtume huyu aliuwawa kwa kukatwa kichwa chake.
MTUME PHILIPO
Mtume philpo alihubili maeneo mbalimbali, aliuwawa kwa kusulubiwa msalabani
MTUME ANDREA
Kuhusu huyu mtumishi soma yohana 6:9 yohana 12:22
Mtume huyu alihubili injili katika inchi ya ugiliki , alikufa kwa kusulubiwa kwa msalaba wa x yanimbao mbili zilisimikwa chini ya andrea akaangikwa ili afe polepole. Walimfunga kwa kamba ilichukua muda wa siku tatu akafa.
MTUME YUDA WA YAKOBO
Mtume huyu likuwa akihubili injili nakufanya miujizaa alichukiwa kwa chuki kuu na wa Armenia wakamkamata na kumsulubisha. Akiwa msalabani wakamchoma mkuki akafa.
MTUME SIMON MAKANYO
Mtume huyu alikuwa akifany akazi ya kuhubili injili aliwa huko uajemi aliuwawa.
MTUME BATHALOMEYO
Mtume huyu ni moja ya wanafunzi wa mwanzo wa bwana yesu,alihubili injili kama vile india,pathia, Arabia na Armenia, alipo kuwa huko Armenia ndipo alipopata mateso mengi sana kwaajili ya imani ya kiristo na jina la yesu, mtume huyu alikuwa na mke mumoja na watoto wawili wa kike.mmoja alikuwa ni muombaji na mwingine alikuwa mwimbaji.mtume bathelomeyo alivuliwa nguo zote huko armania na kukatwa mshipa wa damu kwenye mkono wake. Kasha damu yake ilikingwa kwenye glasi mbili na kupewa mkewenye mkewe ambaye alikunywa na baada ya kumaliza kunywa damu ya mume wake akasema maneno yaha “mume wangu jipe moyo mimi natangulia kwa baba”kasha baada ya kusema hayo akaangunguka chini akafa.
>Vile wale mabinti wawili walipewa glasi moj moja ya damu ya babayao nao wakasema “baba jipe moyo sisi tunatangulia kwa baba”nao pia wakafa mumoja mumoja.
>baada ya zoezi hilo kumalizika wakaamuua mtume bathelomeyo toka pale alipolala na kuanza kumchuna ngozi yake, baada ya juchuna ngozi yake yote inasadikika alikuwa bado hai hivyo wakaamua kumtundika msalabani, baada ya kuona kwamba hajafa waliamua kuchukua na kumtumbukiza kwenye pipala mafuta ya moto.
MTUME YAKOBO (aitwaye mdogo)
Mtume huyu yakobo anaitwa mdogo ilikutofatisha kati ya yakobo ndugu yake yohana,kifo chake imeonekana katika kitabu cha matendo sura ya 12, alikuwa akihubiri yelusalem.
>aliuuwawa kwa kupigwa mawe huko jelusalem na wayahudi.
MTUME YUDA ISAKRIOTE
Mtume huyu alijinyonga baada ya kuisaliti damu isiyo na hatia,nafasi yake ilichukuliwa na mtume mathia.
MTUME MATHIA
Mtume huyu aliuwawa kwa kupigwa mawe akiwa huko kolosai katika huduma ya injili.
MTUME PAULO
Mtume huyu ni maarufu sana katika miongoni mwa mitume, alipata mateso mengi sana mara nyingi kama kupigwa viboko 39, kufungwa gerezani, kupigwa mawe,
>mtume huyu aliuwawa kwa kukatwa kichwa chake huko rumi.
MWINJILISTI MARKO
Mtumishi huyu aliuwawa kwa mateso kwani alikuwa akifanya huduma ya injili huko misiri, wamisirli walimuonea wivu na kumkamata, kasha wakamfunga kamba miguu yote miwili kisha wakaanza kumburuza barabarani. Kichwa kilikuwa chini na mgongo ukiburuzika chini na ukiendelea kuchubuka na kuchuruzika damu.baada ya mateso hayo makali wakamfikisha gerezani akiwa nyama zake zimekwisha katika mwili wake, kisha wakamuweka gerezani ambako walimwangia mafuta na kisha kumchoma moto.huo ndio ukawa mwisho wa maisha ya mwinjilisti marko.
MWINJILISTI LUKA (Dr Luka)
Dr luka yeye alikuwa tabibu, mtumishi huyu wa mungu inasemakana alifanya kazi ya kuchunga makanisa na kuhubiri sehemu mbalimbali, mtumishi huyu haijulikana kwamba alikufa kwa kifo gani na wapi inasadikika aliasilika na mateso ya kanisa chini ya mfalme nero wa dola ya rumi.
MTUME YAKOBO (NDUGU YAKE BWANA YESU)
Mtume yakobo ni ndugu wa kunyonya wa bwana yesu mathayo 13:55. Mtume huyu alikuwa anafanya huduma yake katika mji wa yelusalemu aliuwawa kwa kupigwa kwa mawe baada ya kupandishwa juu ya mnara wa hekalu la yerusalemu na kuambiwa ajiangushe chini.
MTUME STEPHANO
Alipigwa kwa mawe mpaka kufa, na sauli ambaye ni Paulo alikuwa akishuhudia kifo cha stephano huyu ni moja wa mashahidi wa imani.
Mwangalie ayubu katika mateso yote hakumwacha mungu, Daniel, misheck shadraka na abinego hawa kumwacha mungu, waliinua macho juu ambako msada wa mungu unatoka.
Unaweza kusoma zaidi katika bibiliaya mafunzo ya uzima tele, hollman illustrated bible dictationary,simith bible dictionary
Nb: naamini kwa kusoma habari ya watumishi wa mungu utapata hatua ya kwenda mbele kiimani bira kumwacha yesu. Yesu mwenyewe alisema’’ kama mti mubichi unaweza kutendewa hivi itakuwaje kwa mti mkavu?’’ mtu mkavu ni mwanadamu.pia alisema’’ kama mwenye nyumba ametendewa hivi itakuwaje kwa wakaaji wa nyumba?’’
Ujumbe huu umeandaliwa nami M.samlega Willy mwinjilist na mhubiri,
Kama unashida ya unaweza kunipata kwa mawasiliano hapa chini.
p.o.box 3392
mbeya city-tanzania
email: willyministry@yahoo.com
willhopefoundation@rocketmail.com
simu +255 0762 060641/0713 151874/
Subscribe to:
Posts (Atom)